Monday, January 19, 2015

NI JINSI GANI TUNAYATATUA MATATIZO YETU YA MAHUSIANO..

Katika mwaka huu mpya uliianza jiwekee malengo na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza mbele yako, dhamira yako kubwa iwe kufika pale unapopataka.Hata hivyo, katika kutimiza malengo yetu kuna wakati tutakumbana na matatizo, hii ni kwa sababu matatizo katika maisha ya binadamu ni kitu cha kawaida.
Hakuna anayeweza kuyaepuka na ndiyo maana hakuna anayeweza kupitisha siku bila kukumbwa na tatizo, liwe dogo ama kubwa.

Lakini, utafiti unaonesha kwamba miongoni mwetu wapo watu ambao wanapokumbwa na matatizo hushindwa kuyachukulia kuwa ni ya kawaida, badala yake wanaishia kwenye kuvunjika mioyo na hata kumkufuru Mungu.

Ni wazi kwamba binadamu tunatofautiana katika namna tunavyoyapokea matatizo pale yanapotukabili, lakini baadhi ya watu wanapitiliza katika namna wanavyoyapokea kwani inafikia wakati mtu anapopatwa na tatizo huingia katika hali fulani ya kuona dunia ni mbaya na maisha ni yenye upendeleo.

Anashindwa kuyaangalia matatizo hayo kwa umakini na kuyakubali kisha kuangalia uwezekano wa kuyatatua, matokeo yake sasa tatizo linazidi kuwa kubwa.Katika maisha tunapoingia katika hali kama hii ni sawa na kujizuia kusonga mbele katika kupata ama kutafuta kile ambacho tunakitaka katika maisha yetu ya kila siku.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba hali ya kukata tamaa inapopiga hodi katika nafsi zetu huwa tunashindwa kufanya yale ambayo ni ya muhimu na kuishia kwenye kusononeka.Aidha, wengine wanapopatwa na matatizo badala ya kuyatafutia ufumbuzi hupandwa na hasira na wakati mwingine kuchukua uamuzi ambao haustahili.

Kwa mfano umekuwa katika uhusiano na mtu ambaye ulitokea kumpenda sana lakini ikafikia kipindi ukamkosa, aidha baada ya kufariki ama kuachana. Au fikiria umepata barua ya kuachishwa kazi au kama ni mwanafunzi umefeli katika masomo yako yote, hivi utajisikiaje?

Wapo ambao wamefika hatua ya kukatisha maisha yao kwa kukumbwa na matatizo kama hayo. Lakini je, huo ndiyo ufumbuzi sahihi? Hatuoni kwamba kwa kufanya hivyo ni sawa na kumkufuru Mungu?
Wengi wetu tunapokuwa katika matatizo tunaona kwamba maisha yamefika mwisho, tunaona Mungu ni mwenye upendeleo ama tunapopatwa na matatizo, Mungu anatuadhibu, dhana ambayo haina ukweli ndani yake.

Ndiyo maana kuna wakati unaweza kumkuta mtu anapokumbwa na tatizo fulani akasema; “Maskini mimi, nimemkosea nini Mungu.” Anasema hivyo kwa sababu anahisi yeye hastahili kupatwa na matatizo bali wanaostahili ni wale wakosaji tu.Ukweli ni kwamba, matatizo hayachagui mtu, humtokea kila mtu na wakati wowote lakini pia yana ufumbuzi wake.

Hivyo basi unapokumbwa na matatizo si vizuri kabisa kuanza kunung’unika bali fanya kila uwezalo kutafuta ufumbuzi tena kwa kutumia mbinu sahihi. Ninachopenda kushauri ni kwamba, kama unasumbuliwa na tatizo fulani si wakati wa kukata tamaa na kuona kwamba huna haki ya kuendelea kuishi.

Fahamu unayo nafasi ya kukabiliana vilivyo na matatizo hayo. Elewa unapokabiliwa na tatizo fulani kisha ukashindwa kutafuta ufumbuzi, unaweza kulifanya tatizo likawa kubwa zaidi ama kuzua tatizo lingine.

Saturday, January 17, 2015

HATA WANAUME NAO HUCHEZEWA NA KUACHWA.

Wanateseka kama wanavyoteseka. Wanapata tabu na matatizo ya moyo sawa na wanawake. Hata hivyo, wengi hawapati nafasi ya kuwaelezea.

Imekuwa ni kawaida sana kusikia wanawake wakilalamika baada ya kuachwa au kuachana na wapenzi wao, kwamba wamepotezewa muda, wamechezewa n.k. Hizi zimekuwa kauli za kawaida kabisa katika jamii, lakini ukitazama kwa upana dhana hii ina matatizo kidogo.

Hebu tujiulize pamoja, kuchezewa ni nini haswa? Kwanini wanawake wamekuwa na tabia ya kulalamika kwamba wamechezewa? Ni kweli kwamba wanaume nao hawawezi kuchezewa na kuachwa? Bila shaka yoyote, majibu ya maswali haya utayapata katika mada hii ambayo itakuongezea jambo fulani kichwani mwako.

DHANA YA KUCHEZEWA
Inawezekana kila mmoja akachambua kwa mtindo wake, lakini mwisho maana inabaki katika mlengo mmoja tu, kupotezewa muda, kutumika kimapenzi! Hiyo ndiyo maana ya moja kwa moja.

Kama ndivyo, mwanaume ana kitu gani cha tofauti katika mwili na moyo wake, ili aondolewe kwenye kipengele cha kuchezewa na kuachwa? Wapo wanaume ambao maisha yao yamebadilika baada ya kuachana na wapenzi wao waliowapenda.

Hata wanaume nao huteswa, huteseka na hushindwa kufanya mambo mengine, pindi wanapochukua uamuzi mgumu wa kuachana na wale ambao wanawapenda kwa dhati.

HISIA
Naomba niwatoe mchanga machoni kuwa, hisia za mapenzi ni zile zile. Haina maana kwamba, mwanamke ana uwezo wa kupenda sana kuliko mwanaume, la hasha! Kikubwa ni hisia kuwa za kweli.
Kwamba mwanamke kama atakuwa hajampenda mwanaume kwa dhati, kadhalika na mwanaume naye akiwa hajampenda mwanamke kwa dhati, itabaki kuwa hivyo, lakini kama wote watakuwa na mapenzi ya kweli, hali hiyo itaendelea kuwa hivyo kwa wote.

KUWEKEZA MAPENZI
Kama ulikuwa hujui, anza sasa kuingiza jambo hili kichwani mwako, kama wafanyabiashara wanavyowekeza katika sehemu mbalimbali, ndivyo ilivyo pia katika mapenzi. Mwanaume kama alivyo mwanamke, akipenda kwa dhati huhifadhi moyo wake kwa mwanamke huyo.

Mapenzi ni kuwekeza na ukishafanya hivyo, inakuwa vigumu sana kuuondoa moyo wako. Hapo sasa ndipo yanapokuja maumivu na dhana ya kuchezewa na kuachwa!

UKIYAFAHAMU HAYA,UTAEPUKA KUSALITIWA.

1.AMINI HAWEZI KUKUSALITI.
Jambo la kwanza kabisa ni kujenga imani kwamba mpenzi wako anakupenda, anakuheshimu na kukuthamini hivyo hawezi kushawishika kwa namna yoyote ile kukusaliti.

Hii itakufanya kuwa na furaha na yeye, pia utamfanyia mambo ya kumfurahisha. Ukiwa huna imani na mpenzi wako, unaweza kujikuta unapunguza mapenzi kwake na matokeo yake ukachochea yeye kuanza kukusaliti.

2.MTOSHELEZE.
Mpenzi wako mchukulie kama mtoto. Unapomlisha unahakikisha ameshiba ndiyo unamuacha. Akitaka pipi unamnunulia. Vivyo hivyo kwa mpenzi wako. Mtoshelezea katika kila nyanja.

3.Muoneshe upendo wa hali ya juu, mpe heshima anayostahili na pale mnapokuwa kwenye mambo yetu yalee, mpe hadi aseme nimeshiba mpenzi wangu. Ukifanya hivyo aende nje kutafuta nini? Akienda, huyo ana tamaa zake za kijinga na ukibaini muache haraka.

4.ZUNGUMZA NAE.
Ndiyo, vunja ukimya, zungumza naye! Si vibaya ukawa unazungumza na mpenzi wako juu ya mambo yahusuyo uhusiano wenu. Muulize ni mambo gani ukimfanyia anasikia furaha, akikuambia na mambo hayo yakawa ndani ya uwezo wako, jitahidi kumtimizia.

5.Muulize, anachukizwa na mambo gani, akikuambia basi jiepushe nayo. Hata asipokuambia, ukimchunguza utayabaini tu.
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo ukiyazingatia yanaweza kukusaidia katika kumfunga ‘spidi gavana’ kimtindo mpenzi wako ili asikusaliti. Kama itatokea akakusaliti licha ya kumfanyia yote hayo, huyo siyo mtu wa kuendelea kuwa naye.

PENZI LAKO LIMECHUJA,UNAJUA CHANZO?

Leo nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja.

Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana.
 
Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hayo.
 
Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi  alivyo fundi wa 'kuyarudi' ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.
 
Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni lakini tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out' mara tatu katika kumbi tofauti za starehe na kufurahia mapenzi yenu, hali hiyo itabaki historia tu.
 
Hivi hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zile naanza uhusiano na mpenzi wangu mapenzi yalikuwa moto moto, kila wiki ilikuwa lazima twende beach lakini, siku hizi nikigusia tu kwenda huko ni ugomvi."
 
Maneno kama haya huwa yananiuma sana hasa ninapogundua kwamba walio wengi wanakuwa na nguvu ya soda pale wanapoingia katika uhusiano lakini baada ya muda mambo hubadilika kabisa.
 
Sijajua ni kwasababu gani lakini kwa utafiti mdogo ambao nilioufanya kwa baadhi ya wanaume ni kwamba, wao wanapofanikiwa ‘kuona ndani tu’ hujenga kiburi fulani kwa wasichana wao huku wakiamini kwamba, hata wawe tofauti vipi hawawezi kuachwa!

Labda nijaribu kushauri kitu katika hili kwamba, kama uko kwenye uhusiano wa kimapenzi ama uko ndani ya ndoa, unatakiwa kufanya kila linalowezekana kulifanya penzi lenu lisichuje.
 
Wewe ndio unaweza kulifanya likaendelea kuonekana kuwa jipya kila siku ama kulifanya likachuja mithili ya nguo inayochuja rangi iliyotumbukiza katika ndoo ya maji ya moto.
 
 
Hatukatai kwamba, kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi wake wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora ya baadae, si unajua tena mnapokuwa na malengo ya kimaisha zaidi?
 
Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, penzi la dhati haliwezi kuchuja hata siku moja. Tujue wapo ambao wameishi miaka zaidi ya hamsini lakini penzi lao bado ni moto licha ya kuwepo kwa mabadiliko madogo ambayo hayakwepeki kutokana na umri.
 
 
Yapo mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe, tukumbuke kwamba baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo huko nyuma ndivyo viliwavutia wepenzi wetu na kukubali kuwa nasi kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.

Friday, January 16, 2015

ZIJUE DALILI ZA UHUSIANO WENU KUPOTEZA UELEKEO.

1. MAWASILIANO KUWA DUNI
Mapenzi na sawa na jani la mti. Huendelea kuwa na mawasiliano na shina kwa kusaidiana na matawi. Ila siku ikifika jani linadondoka. Hii utokea pale jani linapochoka na maisha ya kujishikiza. Haya ndiyo sawa yalio kwetu binadamu. Mwanzo uanza kwa kasi zaidi na mwisho hufifia kwa mawasiliano. Mtu anaweza kukata mawasiliano kwa sababu zake binafsi zikiwemo hizo za hapo juu.
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara tano kwa siku (kwa wale walio mbali, mfano masomoni.), basi mawasiliano yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi mwisho wa siku mawasiliano kukaka kabisa. Hapa kila mmoja akiulizwa swali kwanini husema nilibanwa na kazi ndio maana sikuweza kukutafuta.
Kwa walio kwenye ndoa mawasiliano pia yanakuwa nyuma kidogo. Kama alikuwa anakusalimia kwa kukumbatiana, hapa hali hua tofauti kabisa. Muda mwingine kila mtu na kazi yake. Kila mtu shuka yake, na kukicha kila mtu kivyake.
Hii hua na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine. Yule ambaye ulidhani umemchagua anakuja kuwa sumu kwako. Unapenda umwone yeye ataki. Unapenda umpe zawadi yeye ataki, unapenda kutoka naye out yeye ataki, na pale anaposema uwasiliane naye basi roho huweka pembeni. Utagundua kuwa kama analazimishwa aongee.
Ikifikia sehemu hii na kama ulimpenda kweli basi utaongeza jitihada za kutaka kuwa naye, wasio na imani hufikia mahali wanasema nitaendelea kukaa bila kuoa. Kauli hii ni udanganyifu tu. Akisahau yale yaliyomtokea, anaamua kusaka mke au mume mwingine. Unapoona hali hii imeanza jalibu kuwajilazimisha kuwa karibu yake sana. Na pale unavyoona hali ni mbaya zaidi basi mweleze rafiki yake wa karibu ambaye humwamini kwa kila jambo.
Au unaweza kumweleza mtu anayeheshimika ili asikilize kilio chako na mwisho wa siku utaona mafanikio. Hii ni kwa wachumba na hata kwa wanandoa itapotakiwa kufanya hili.
Kwa wanandoa ni muhimu wawaone pia wezee wa busara ambao wanaaminika na kukubalika na jamii. Ikishindikana basi waende katika ofisi ya kata au ustawi wa jamii kwa msaada zaidi.
 
 
2. USO HUONYESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
Ni hali ya kawaida kuona mke au mme kuonyesha kuwa apendi kuongea na wewe. Sababu kubwa anayo moyoni na hataki kuisema. Uso mara nyingi unakuwa na asili ya mkunjo kwa wanawake. Na kwa wanaume sura inakuwa na asili na makunyanzi. Hapo ujue kuwa hali ni mbaya sana. Hapo hata ukimsesha anaona kama unajisumbua tuu. Na kama ataamua kusema ni kidogo tu na mwisho inaedelea kukaa kimwa.
Pia hata majibu yake uteyaelewa tu. Ni ya unyonge hivi, na sauti ya chini isiyo na mvuto au ushawishi kwa mwenzake. Pakifikia mahali kama hapa jalibu kumnunulia zawadi mzuri, kumkisi, kumwambia oooo mpenzi wangu….nakupenda sana…….leo umependeza namna hii….. Kweli mimi nimechagua mke mzuri au mme mzuri sana……kwani najivunia sana kukuona na kuwa na wewe muda wote.
Wakati mwingine unaweza kwenda kumsaidia kupika, kuosha vyombo na hata kumwambia mkaoge pamoja. Utaona jinsi anavyoanza kubadilika mpenzi wako. Hapa hakuna mchawi bali ni namna tabia yako ulivyomwonyesha. Hali hii haiwezi kwisha ghafla kama kimbunga bali huenda taratibu na mwisho wa siki hali inajirudia. Kwa hali ya kawaida uchukua kuanzia siku 21-22. Uendelea kumwambia maneno yenye baraka na busara bila ya kukata tama. Uwe na imanii ya hali ya juu kwani majibu utayokutana nayo si ya kawaida, lakini mwisho wa siku hali itarudi kuwa ya kawaida kabisa.
 
                                
  
3. HASIRA ZAMARA KWA MARA.
Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake ni baya. Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti. Mfano wa majibu utayokutana nayo ni kama haya:-
mbona hivi mpenzi?
mimi nifanyaje?
Wewe yanakuhusu nini?
Umepata hasara gani mimi kufanya hivi?
Fanya utakavyo?
Mimi ndo kila kitu?
kwa nini yamefikia hapo?
we ujui?
Hizi ni baadhi ya changamoto utazokutana nazo wakati wa maojiano yako na mpenzi wako. Usimpige kisa majibu ya mkato. Kama mwanaume hali ikizidi kuwa ni kelele tu, basi kaa kimya au ondoka na kwenda kufanya shughuli zingine. Utavyorudi atashindwa anzie wapi.
Kama ni upande wa mwanamke yanamtokea haya basi fanya hivi:- kaa kimya kwa muda, atakaa kimya mpenzi wako. Kasha usisite kumwandalia mmeo chakula cha kutosha na kizuri. Hata kama hali usichoke kuandaa. Mpe maneno matamu mkiwa kitandani na kujaribu kumgusagusa sehemu mbalimbali za mwili. Hapa mwanaume ujanja unaisha hapo.
Kama hizo njia zinachukuwa muda mrefu basi anza kwa kumuomba msamaha. Hata kumpigia magoti usione aibu. Piga huku ukionyeshwa kuwa hali hile upendezwi nayo. Ni ya bahati mbaya. Hakirudi katika hali ya kawaida na siku nyingi kupita anza kushusha makombola kwa njia ya utani kuwa pale mme wangu kosa lilikuwa lako. Kama muelewa ataweza kijirekebisha ipasavyo na mwisho wa siku mukarudi kama siku ya kwanza kuanza penzi lenu.
 
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
Hii ni hatua ya nne ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi wako hutamuona mchungu kupita kiasi. Hutaona kama kuna watu wanamfundisha kuongea maneno haya. Ukweli ni kwamba ukishaona mke wako mara nyingi yeye na wenzake, hana muda wa kukaa akuandalie chakula (kwa mwanamke aliye kwenye ndoa) basi ujue kwamba rafiki zake wamemfundisha na ujue kuna jambo linaendelea ambolo mwisho wake ni kutengana.
Kwa mchumba basi utaona maneno ya ovyo ovyo ili mradi umwambie sasa mimi na wewe basi. Atafanya kila aina awezavyo utengane. Hii huweza kuwa mwanaumme ndio kisa au mke mwenyewe ndio kisa. Akishindwa hapa anaamua kuchukuwa maamuzi magumu sana ambayo hutasahau tena maishani. Kama vile kumpigia mpenzi wake mpya na kuanza kuongea naye.
Hiyo atakuwa amekuheshimu, anamkumbatia na kumkiss ili mradi uhuzunike kwa hili kasha mtenge ili awe huru. Hali hii huwa ni mbaya zaidi kama mtu umependa. Hhiki ni sawa na wanavyofanya wanaume walio wengi katika uchumba na doa. Ukimuuliza namba hii uliyosevu Juma mbona inaonyesha ni hile ya Asha atakuambia ni rafiki yangu.
Ukiendelea kumbana atakuambia ni ya mke wangu. Sasa wewe unasemaje au unataka nini? Haya utokea kwa wote wenye ndoa zao na wale walio kwenye uchumba bila kujali mme au mke au mchumba.Haya ndiyo yanayojili sehemu hii iwapo utashindwa kutatua hizo hatua tatu za mwanzo.
Namna ya kutatua sehemu hii ni kutumia zile njia elekezi ya hatua ya kwanza. Kubwa zaidi hapa ni kuomba msamaha kwa kile kinachovumilika, na kile ambacho akivumiliki ni kwenda kwa washauri nasaha kama vile maafisa ustawi wa jamii kwa manufaa ya wote. Wao watakusaidia vizuri hata kama uko peke yako na mwenza wako alikataa kwenda huko. Utamsahau na kuiona dunia ni tamu zaidi y asana na utasema mwenyewe ulichelewa wapi kipindi yanatokea haya.
 
                           5. KUDAI KUTENGANA
Kama mnavyojua, mti uota, ukua, utengeneza majani, huishi na hatimae mwisho kufa. Hapa mpenzi wako utaona ni balaa tupu. Yaani hafai hata kidogo. Kama una imani ndogo utatamani uondoke uende mbali ambako hutamwona tena. Hapa hakuna jinsi, hata mahakama huamua kutenganisha ndoa kama walioana. Hapa usipofanya kama atakavyo mpenzi wako unaweza kuishia hata gerezani au kuchukua uamuzi wa kumpiga.

Kweli inauma sana kumwona mke/mme au mchumba unaempendaanataka mutengane. Wengine huamua kujinyonga, wengine kunywa sumu, wengine wanaamia baa na kuweka makazi yao. Mmoja hakikataa hakuna jinsi, mwache aende kwa usalama.
Jinsi ya kutatua hili ni kwamba unapaswa kwenda kukubali tatizo lililotokea. Kwani kinachotokea kwa wenzako hata wewe ipo siku yatatokea. Katika maisha ya binadamu kuna kupenda na kutendwa, hivyo kutengana ni moja ya sehemu ya maisha. Jaribu kutembelea sehemu zenye mkusanyiko wa watu. Lakini usinywe pombe, na kama ulikuwa unakunya unaweza kuacha kabisa hatakwa miezi kadha na usitembelee sehemu za pombe.
Unaweza kwenda disco na sehemu nyinginezo mzuri kama vile kwenye mpira, kucheza puru, drafti, bao na hata karata. Hali yako itarudi kama zamani. Utajiona wa kawaida (hii ni kama kwa mwanaume). Ukikutana naye usimwone kama ni adui ako mkubwa, kwani yaliyotokea ni majaribu ya dunia. Na pale mkaapo kwa muda mrefu na kuona kuna umuhimu wa kurudiana basi murudiane kwa moya mmoja.
Kwa wanawake huchukua muda mrefu kama tendo lilifanywa na mwanaume. Na tatizo lenyewe kama kumfumania mme au mchumba wake wakiwa katika chumba kile kile anacholala yeye. Huwa anaona ni unyama. Kwa hili, mke huyu kurudiana naye itachukua muda mwingi kwani lile swala humrudia mara kwa mara. Na kama alimpenda sana bwana wake huamua usikuone kamwe.
Lakini hakuna jambo lisilo na mwisho. Mme unapaswa kwenda kuomba msamaha kwa yule mke wako uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni jambo la kawaida, kwani ile icha itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii, fanya hivi zaidi ya mara tano hadi kumi. Mke wako au mme wako ataanza kukuonea huruma na hatimae kuwa naye pamoja.

HAYA NI MAMBO YA MSINGI YA KUMFANYIA MPENZI WAKO.

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.

Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.
Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.
Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI
Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako.


Thursday, January 15, 2015

WIVU NI CHACHANDU YA MAPENZI,LAKINI UKIZIDI SANA HUWA KARAHA.



WOTE tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutufikisha siku hii.
Kama kawaida tunaendelea na mada nyingine ya jinsi unavyoweza kuudhibiti wivu wako. Hakuna asiyejua wivu ni nini hasa katika suala ya uhusiano. Kila kiumbe chenye akili timamu lazima kiwe katika hali hiyo.

Wivu wa mapenzi unamaanisha nini?
Wivu katika mapenzi unamaanisha mtu kumiliki mpenzi wake peke yake pasipo kuingiliwa na mwingine, kwa maana nyingine kuonyesha unampenda na kumjali ila ukizidi unakuwa sumu.
Kiumbe kisicho na wivu ni sawa na mwili bila roho ambacho lazima kitakuwa ni mfu.

Lakini kwa kiumbe kinachovuta pumzi lazima kiwe katika hali hiyo na kama huna huku bado unavuta pumzi basi hujui nini maana ya kupenda. Lakini kwa yeyote anayeijua thamani ya kupenda lazima atakuwa anajua maana ya wivu.

Wivu katika mapenzi ndiyo chachandu kwa mtu kujua kweli anapendwa. Huwezi kuwa na mke au mume akichelewa au kusimama mazingira yasiyo eleweka ukae kimya, ujue lazima kuna walakini akilini mwako.

Lakini leo nataka kuzungumzia wivu uliovuka mipaka ambao huwa kero kwa wengine. Wapo wanaume au wanawake huwaonea wivu hata dada au kaka yako.

Katika suala hili napenda kulieleza kwa mapana kwa ajili ya kwenda pamoja ili tuweze kupunguza wivu ambao umekuwa kero kwa watu hata kufikia kuvunja uhusiano. Jambo hili niliwahi kulizungumza awali kuwa hakuna kiumbe anayewaza ngono kila, wakati ukiona hivyo ujue ana matatizo.

Pia nilielezea kusomana tabia kabla ya kuanza uhusiano na siyo kukutana kimwili ndiyo msomane, kama wengi wasemavyo.
Kusomana tabia ni pamoja na kujua historia ya nyuma ya mwenza wako, ukizijua tabia zake naamini ukimwonyesha njia utatumia muda kuyarekebisha matatizo yake huku ukimweleza sababu ambazo huenda zitasababisha msiwe pamoja.

Mkirekebisha tatizo hilo ni wakati wenu kuanzisha mapenzi mkiwa mnajuana, kila mmoja anaujua udhaifu wa mwenzie ambao unarekebishika.
Usimpende mtu kwa ajili ya sura au umbile, lakini ikiwa tabia yake ni mbovu huwezi kuibadili kama ilikushinda mkiwa na uhusiano wa juu juu.

Unajikuta unakuwa na wivu wa kijinga hata ukimkuta mpenzi wako amekwenda sokoni dukani au kwenye maji wewe unajua amekwenda kwenye ngono.
Unaweza kuuthibiti wivu wako wa kijinga kwa kuitengeneza tabia ya mwenzi wako ambayo utaijua vizuri kitu kitakacho kufanya umjue vizuri mwenzako na kuweza kumuamini.
Narudia tena hakuna binadamu anayewaza ngono kila wakati, peaneni uhuru ili kujengeana uaminifu.

Pia hata unayetumia mwanya kwa ajili ya kufanya uchafu wako. Jifahamu kuwa wewe si mnyama ni mwanadamu unayetakiwa kujiheshimu, mwili wako anayetakiwa kuujua ni mwenza wako tu.
Uhuru unaopewa usiutumie vibaya na kusababisha kuwaingiza mwenzako kwenye kapu la samaki waliooza na kuwafanya wote waonekane wameoza. Kama bado unataka kufanya uchafu wako usikubali kuingia kwenye uhusiano wa kujenga familia.

EPUKA KUPOTEZEWA MUDA WAKO.

Kujifunza, kuelewa na kufuata ni kitu kizuri kwa mtu mwenye hulka ya kupanua mawazo yake. Hakuna aliyekamilika, Kila siku watu wanakosea. Hakuna mtaalamu wa kudumu wa mapenzi.

Kwenye mapenzi tunazidiana uelewa tu. 
Leo tuijadili hii mada.Ni kuhusu wanawake wanavyopotezewa muda na wanaume ambao hukaa nao muda mrefu katika uchumba unaishia hewani.
  Ki ujumla si sahihi sana kukaa kwenye urafiki kwa muda mrefu. Usidanganyike na pete, mwenzi wako anaweza kubadili mawazo wakati wowote. Uchumba wa muda mrefu lazima uwe na sababu maalum, labda masomo n.k.

Kama umepata mchumba, kuna mambo muhimu tu ambayo ukiyachunguza na kujiridhisha, mnatakiwa kuingia kwenye ndoa, bila kusubiri zaidi. Hebu tuone mambo hayo.

MAMBO YA MSINGI KUCHUNGUZA .

1. UNAMPENDA KWA DHATI?

Tiketi ya kwanza kwenye uhusiano ni kupenda. Lazima ujihakikishie kuwa mwanaume uliye naye unampenda na nafsi yako imeridhika.

2. ANAKUPENDA?

Chunguza kama anakupenda. Yapo mambo ya msingi ambayo yakionekana utakuwa na hakika kuwa mwanaume wako anakupenda kwa dhati.
Kwanza namna ambayo anapenda ukaribu wenu, anavyokushirikisha kwenye mambo yake, kukujali. Mfano unaumwa, anakuwa karibu na wewe na wakati mwingine hukuchukua na kukupeleka hospitalini kutafuta tiba.

Atapenda kujua kuhusu ndugu zako, hali zao kiafya na mengine ya msingi. Mwanaume wa ukweli, ambaye anakupenda, atahakikisha yeye anakuwa faraja yako na kukuongoza siku zote.
Akiwa na tabia hii maana yake anakupenda.

3.DINI.
Lazima kuangalia suala la dini. Inashauriwa wanaooana wawe wa madhehebu moja ili kuepusha migongano. Mambo ya kiroho yana uhusiano mkubwa sana kwenye ndoa.
Imani husaidia zaidi kutatua migogoro, matatizo ya kuua nk. Haitakuwa jambo zuri, mpate watoto ambao hawatajua wapi panawafaa kuabudu.

Yapo madhehebu yanayoruhusu ndoa za mseto lakini kwa baadaye inaweza kuleta usumbufu. Zungumzeni, kama ni lazima kuoana, mmoja wao akubali kuhamia kwa mwenzake (tena kwa kuamini, si kwa ajili ya ndoa).

4.MILA.

Chunguza mila za kabila lao. Jaribu hata kuwatumia wazee. Kuna baadhi ya makabila yana mila ambazo kwa wengine zinakuwa na migongano. Kuwa na hakika na hilo kwanza.

YA NINI KUPOTEZA MUDA?
Baada ya kuchunguza yote hayo na kujihakikishia, una sababu gani ya kupotezewa muda? Kama umeridhika na hayo, maana yake mnatakiwa kukaa na kujadili kuhusu ndoa, kama hataki ujue si wako.
Ni uamuzi wako mwenyewe, kuamua kupotezewa muda au kuwa makini na maamuzi yako. Ndugu yangu kila kitu kipo vichwani mwetu. Tumepewa uwezo wa kufikiri wote, tatizo ni namna ya kufikiri tu. Shughulisha ubongo wako.

UAMINIFU SILAHA YA KWELI KATIKA MAPENZI.

NI furaha iliyoje kukutana tena katika safu yetu nzuri ya kuelimishana juu ya mapenzi? Sina shaka utakuwa mzima wa afya njema na upo tayari kupata kitu kipya. Nakukaribisha kwa moyo mkunjufu tuongeze maarifa.

Rafiki zangu, leo nazungumza juu ya jambo muhimu sana katika mapenzi; uaminifu. Huu ndiyo msingi wa uhusiano, ndoa na mapenzi. Ikiwa uhusiano utakosa uaminifu, ni wazi kwamba hautakuwa na umri mrefu.

Uaminifu ni jambo lenye mvutano mkubwa, ni mjadala usiokwisha tangu kuwepo kwa mapenzi. Ukweli ni kwamba uaminifu ndiyo kipimo cha kwanza cha kugundua kama penzi lako ni la kweli au moyo wako unakudanganya.

Hata hivyo upo ukweli ambao hauwezi kukwepwa! Uaminifu unawashinda wengi sana walio kwenye uhusiano. Watu wanashindwa kuwa waaminifu kabisa. Pamoja na yote hayo, zipo sababu ambazo zinaelezwa zinasababisha mwenzi kukosa uaminifu kwa mpenzi wake.
Hebu twende tukaone ni kwa nini watu wanakosa uaminifu.

KUKULIA KATIKA IMANI...
Hili ni la kwanza kabisa ambalo unapaswa kulifahamu rafiki yangu mpenzi, malezi ya kiimani! Neno uaminifu tukilinyambua tunapata maneno imani, amini na aminiana. Kwa msingi huo basi, ikiwa mpenzi wako hajakulia katika mazingira mazuri ya kiimani kulingana na taratibu za dini anayoiamini ni vigumu sana kuwa mwamnifu au kukuamini!Hii ina maana kwamba wakati unachagua mchumba ni vizuri kuangalia pia suala la imani ya dini yake.

Je, ni muumini kikamilifu katika imani yake? Maana katika imani za dini, kitu cha kwanza kabisa kufundishwa na kutiliwa mkazo ni uaminifu! Katika uaminifu huwezi kukuta uongo, usaliti, masengenyo na mengine mengi ambayo siyo mema.
Mwaminifu ana hofu, atapenda kuzungumza ukweli siku zote maana imani ya dini yake inamsuta.


UNAPASWA KUWA MWAMINIFU
Ikiwa ni kweli unahitaji kuwa na mwenza wa peke yako, basi lazima uanze kujiamini kwanza wewe mwenyewe. Hili ni jambo la kwanza kabisa kwako, ukikosa uaminifu basi ujue lazima mpenzi wako naye atakusaliti.

Jifunze kuwa mkweli siku zote, kila mmoja anajua jinsi gani ukweli unavyouma lakini unapomwambia mpenzi wako ukweli anajisikia furaha, huru na amani kuwa na wewe. Anajiona bora maana amepata mpenzi mkweli na muaminifu.

Hakuna haja ya kumdanganya mpenzi wako ulipotoka kazini ulipitia kwenye pati wakati ulikwenda kuangalia shoo kwenye kumbi za burudani.

Kumbuka kwamba unaweza kumdanganya na akakuamini lakini kumbe ukiwa huko kwenye starehe zako kuna mtu anayemfahamu mpenzi wako alikuona na akaenda kumwambia, unafikiri akikuambia ulionekana huko itakuwaje?

Lazima atahisi kuna kitu kingine unamficha ulichokuwa ukifanya huko, ingawa pengine hukuwa na kitu kibaya zaidi ya kuangalia shoo ya bendi uipendayo; sasa ili uweze kuzima hisia hizo ni vyema kuwa mkweli. Mweleze tu: “Samahani sweetie, unajua jana nilikuwa nimechoka sana, rafiki yangu akaniomba niongozane naye kwenye muziki, lakini naomba unisamehe sikuweza kukutaarifu mapema.”

Ni sentesi fupi inayoonyesha uungwana wa hali ya juu, uaminifu na kujali uwepo wa mpenzi wako. Hapa unamfanya ajisikie yeye ni maalum kwako.

NI MWAMINIFU KWAKO?
Katika ulimwengu wa mapenzi, hili ni jambo la msingi sana. Huna sababu ya kuwa na mpenzi asiye mwaminifu, sasa ili usije ukaingia katika mkumbo huu ni vizuri kumchunguza lahazizi wako kwa muda mrefu.

Mwekee mitego, chunguza kauli zake, kumbukumbu zake na mienendo yake, ana uaminifu kweli? Maana asiye mwaminifu hupoteza kumbukumbu juu ya mambo aliyoyafanya.

Hata kama unampenda kiasi gani lakini kama umegundua hana uaminifu ni vizuri kuachana naye mara moja. Mpenzi asiye mwaminifu wa kazi gani? Sana sana atakusababishia presha bure!

JIAMINISHE
Ikiwa ni kweli unampenda mpenzi wako kwa dhati basi inabidi ukubali kuwa katika himaya yake kiuaminifu. Hii ina maana kwamba, mwenzi wako ana uhuru wa kukuchunguza atakavyo ili aweze kuwa na amani ya moyo wake kwako.

Umpe uhuru wa kuishika simu yako na ikiwezekana kuikagua na kukuuliza maswali kuhusu chochote kilichomo katika simu yako. Kama ‘umesave’ picha ya mtu wako wa nje, akaiona na kukuuliza ni kwa nini unayo hiyo picha kwenye simu yako uwe na sababu za maana za kumweleza!
Huwezi kutaka uaminifu katika penzi lako kama wewe mwenyewe hutaki kuwa katika himaya ya uaminifu.

ANZA KUWA MWAMINIFU!
Ni kweli kwamba kipengele kilichopita ni kigumu sana hasa kwa wanaume wenzangu lakini kama ni kweli una mapenzi ya dhati kwa patina wako inakubidi ukubaliane nacho. Silaha pekee ya kuweza kuwa huru na kipengele hicho ni wewe mwenyewe kuwa MWAMINIFU.

Anza sasa kuwa mwaminifu na utafurahia mapenzi ya kweli kutoka kwa mpenzi wako. Inawezekana kuna vitu vingi ulikuwa ukivikosa kwa mpenzi wako, lakini kumbe tatizo lilikuwa dogo sana, uaminifu! Kwa nini uaminifu ukushinde? Inawezekana kama utauachia moyo wako kikamilifu kwa mwenzi wako. Chukua hatua.

posted from Bloggeroid

UTAMJUAJE MWENYE MAPENZI YA DHATI?



Nimeandika mada hii kutokana na watu wengi kushindwa kutofautisha kupendwa kweli na kutamaniwa. Wapo walioingia mkenge kwa neno hilo hasa walio wageni katika uwanja huu wa mahaba. Ukiambiwa unapendwa basi unachanganyikiwa na kusahau maneno matupu hayajengi nyumba.

Nina maana gani?

Watu wengi wamekuwa wakitumia neno hili kama mtego wa kumpata mtu, kwa kujifanya anakupenda sana na nahau nyingi za mapenzi ambazo zinaweza kukufanya masikio yako yazibe na kuona nani kama wewe.

Siku zote mtafutaji ana lugha tamu ya mapenzi na kabla ya kutamka lolote lazima atangulize nakupenda sana na kuongezea ajuavyo. Hii si mara moja watu kuingia mkenge inapotokea wanakutana na hali hiyo.

Lazima uelewe serikali ya mwili wako inakutegemea wewe, ukiipeleka vibaya lawama zitakuwa juu yako. Usiwe na papara ya kutoa uamuzi wa kukubali uambiwavyo unapendwa bila kufikiria kwa kina. Hakuna hata siku moja mtu anayekutaka kimapenzi akuambie anakuchukia.

Fikiri kabla ya kutenda na kuona kauli uliyopewa ina nia gani na wewe, kweli anakupenda au anataka kukuchezea na kukuacha.

Katika uchunguzi wangu nimegundua wengi hupima kwa masikio juu ya kile aambiwacho na si kufikiria nini hasa kilichomvutia aliyekutamkia maneno hayo. Japo kakutamkia anakupenda, ni vema ukafanya kadiri uwezavyo kupata muda kufikiria kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wowote ambao unaweza kukufanya uwe na faida au hasara.

Neno nakupenda siyo mapenzi kamili, bali tabia ya mtu na kuonyesha kweli anakupenda kwa dhati. Akupendaye huwa hana haraka ya kufanya ngono, hufuata taratibu zote ili mradi kujenga uaminifu moyoni mwako.

Hii hutokana na kuwa na uhakika wewe ni wake, hana hofu ya kutanguliza ngono mbele katika uhusiano wenu wa kimapenzi. Ukiona umekutana na mtu anayetanguliza ngono baada ya neno nakupenda huyo hakupendi bali anakutamani.

Tumekuwa tunatumia neno nakupenda kama kiwakilishi cha ujumbe wa mapenzi na si penzi kamili.
Mapenzi ya kweli ni ya vitendo na si maneno, anayekupenda utamjua tu wala hajifichi. Atakuwa mpole, mwenye huruma, anayekujali, muaminifu na mtu aliye muwazi mwenye kukupa uhuru wa kumjua kwa undani ili kukuondoa wasiwasi.

Mapenzi mengi ya siku hizi yamekuwa ya usiri mkubwa yenye mipaka. Kama kweli anakupenda kwa nini akudanganye na akuwekee mipaka ya kumjua? Wakati huo mdomoni kwake ana kila nahau tamu za kimapenzi na kulitamka neno nakupenda kama kiwakilishi.

Huyo si mkweli wala hana mapenzi bali ni muongo aliyejificha nyuma ya neno nakupenda. Kuwa macho na watu hawa.


Posted via Blogaway

Wednesday, January 14, 2015

UNAWEZA UKAWA UNAMPENDA SANA ASIKUPENDE,FANYA UAMUZI SAHIHI.


UHUSIANO  wenye amani na masikilizano ndiyo kitu ambacho kila mmoja wetu anakihitaji na ikiwa hivyo unaweza ukajikuta unanawiri tu!   Wakati mwingine unaweza hata kujikuta hujala chochote lakini ukajihisi umeshiba eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa naye karibu tu, yaani yeye kwako ndiyo mambo yote, yeye ndiyo kila kitu kwenye maisha yako! Huo ndiyo utamu wa maisha!   Naamini kabisa wapo ambao wako katika aina hiyo ya mapenzi na hao wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuwaweka kwenye mazingira hayo.   Lakini sasa wakati wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wengine wanaoishi na wapenzi wao huku mioyo yao ikiwa imesinyaa, yaani hawana furaha kabisa!   Kwao kila siku ni karaha na vituko vya makusudi kutoka kwa wapenzi wao licha ya kwamba wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote.   Cha ajabu sasa, licha ya baadhi ya watu kutokuwa na furaha katika maisha yao ya kimapenzi eti wanahisi njia sahihi ni kuvumilia huku wakiamini siku moja mambo yatabadilika. Jamani, huenda nikawa na msimamo tofauti kidogo kwani mimi naamini mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzio na kuheshimu hisia zake, hasa kwenye mambo yanayofaa.   Tofauti na hapo, tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati.  Mapenzi, nijuavyo mimi ni kupenda,  kupendwa, kusikilizana, kupatilizwa na kuheshimiana na si kinyume chake!   Wakati mwingine unaweza kujikuta katika wakati mgumu wa kuamua hatima ya uhusiano wako na mpenzio kwa kuwa unahisi unampenda sana na kwamba hauko tayari kumkosa.   Ukweli ni kwamba, hata kama huyo uliyenaye unampenda vipi lakini kama anaonesha kubadilika na kutokupa ile furaha uliyotarajia, huna sababu ya kumng’ang’ania. Muache aende zake kwani huenda kuendelea kuwa naye ndiyo kuyafupisha maisha yako.   Inawezekana kuna mambo mazuri ambayo amekuwa akikufanyia huko nyuma kiasi kwamba ukikumbuka unasita kufanya maamuzi ya kumtosa. Sikiliza nikuambie kitu, unapokutana na hali hiyo elewa ni shetani ambaye anataka kukufanya uendelee kuwa kwenye utumwa wa mapenzi.   Pata ujasiri, yaliyopita katika uhusiano wako, yafanye kuwa historia kisha fanya uamuzi sahihi. Uamuzi sahihi ni upi? Sidhani kama hapa panahitaji darasa zito. Uamuzi wa kwanza ni kukubali kuendelea kuwa kwenye uhusiano huo. Utaamua hivyo kama utaona kwamba uko tayari mapenzi yakuue lakini siyo kumuacha huyo uliyetokea kumpenda. Ila kumbuka wanaochukua uamuzi huu ni malimbukeni wasiyoyathamini maisha yao.   Uamuzi mwingine ambao naona ni sahihi ni ule wa kumuacha aende kisha wewe uyaache maisha yako yaendelee kuwepo. Amini bila kuwa naye bado maisha yako yanaweza kuendelea kuwa ya furaha na wala huwezi kujuta. Utajutaje wakati alikuwa akikunyima furaha uliyoitarajia?