Tuesday, May 31, 2016

AINA YA MABUSU NA JINSI YA KUBUSU.

Ukweli busu ni kitu kinachoshangaza hasa kutokana na raha yake, wengi hufurahia sana kutoa na kupokea busu na bado tunakumbukumbu halisi za busu la kwanza lilivyokuwa.
Inawezekana na wewe ni moja ya wale wanaotafakari ladha ya busu la kwanza itakuwaje, Please relax kila jambo na wakati wake na majira yake.
JINSI YA KUBUSU KATIKA BUSU LA KAWAIDA

Angalia machoni kwa mpenzi wako:
Kwamba anategemea kumbusu lazima uelekeze macho yako kumuangalia yeye,
“Eyes are windows to personal soul”
Ukimwangalia usoni utajua kama anahisia (feelings and emotions) kwamba yupo tayari na anakupa ujumbe unaoelekeza kwamba yupo tayari for intimacy.
Pia kumuangalia usoni na kwenye macho yake ni kupeleka ujumbe kwamba unataka kumkaribia kwa ajili ya busu.

Tabasamu
Tabasamu kidogo hupendekeza unataka kufanya kitu, kama unataka kujua kama partner wako anataka kiss unapotuma ujumbe kwa kutabasamu utajua kama yupo tayari au la.
Kama aki-respond kwa tabasamu unaweza kuendelea na ukiona anaangalia chini au pembeni au hali fulani ya kuonesha hayupo tayari unaweza kuacha.

Karibia kabisa
Sasa unajua unataka busu, ni wakati kuelekea kwenye tendo lenyewe, karibia polepole na wakati unazidi kuwa close hakikisha huna papara

kama ni mwanaume unaweza sasa kumgusa au kumshika (hold) mwili wake au uso wake huku ukikaribia polepole na hapo atajisikia kama vile yupo tayari na comfortable.
Elekeza kichwa chako ili midomo iwe rahisi kukutana kwa ajili ya kubusu.
Pia hakukisha upo usawa wa partner wako ili wakati una busu iwe sawasawa usije ukamiss

Relax lips zako, Hakikisha lips zako zipo relax na hazipo tight kabisa na zake, kutanisha lips kwa ulaini kabisa bila nguvu
Hakikisha lips zako siyo kavu.
Kwani lips kavu hazileti raha yenyewe.
Wengine hupenda kufumba macho na wengine hawapendi.
Kwa leo fumba macho na ukishakutanisha lips achia hisia zimalizie kila kitu

BAADHI YA AINA ZA MABUSU

Butterfly kiss
Huku uso upo distance zero na mpenzi wako, fungua kope (eyelids) za macho funga fungua kwa speed huku unagusisha kwenye shavu lake.
Hili ni busu lisilohusisha lips na hutoa mtekenyo wenye kusisimua kwenye shavu.

Eskimo kiss
Huku mpo distance zero na mpenzi wako sugua pua yako kwenye pua yake kama sekunde 10 hivi, raha sana.

Finger kiss
Wakati mmelala wote na mpenzi wako, chukue kidole kimoja cha mkono wake na kubusu kwa kukinyonya.

French kiss
Hili ni busu linalohusisha ulimi wengine huita “soul kiss” kwa sababu uhai na nafsi hupita kwenda kwa mwingine kupitia kupumua kwa kinywa kupitia ulimi “wet”
Kitu cha kushangaza ni kwamba wafaransa huiita “English kiss”
Huhusisha maeneo yote ya mdomo na husisimua maeneo yote ya mwili.

Fruit kiss
Chukua kipande cha tunda (hasa fruit juice kipande cha nanasi, embe au zabibu) ng’ata nusu na yeye nusu na kunyang’anyana hadi linavunjika na juice kutelemka midomoni romantically.

Tiger kiss
Kama tiger huku akiwa hajui ukiwa mgongoni mshike na kumbusu kwa kung’ata shingo (angalie usijemuumiza mimi simo nazungumzia kung’ata kimahaba)

Angel Kiss
Ni tamu, kumfariji kwa kumbusu kwenye lips delicately.

Earlobe Kiss
Polepole ingiza ulimi kwenye masikio na kuyanyonya, usifanye kwa kusababisha sauti sana kwani masikio ni sensitive sana kwa sauti.

UMUHIMU WA BUSU..


Busu husaidia kuwezesha moto wa mahaba kuendelea kuwaka kati ya wapenzi.
Kumbuka mpenzi wako huhitaji kujisikia yupo appreciated na zaidi anapata mapenzi (love and affection) kutoka kwako na njia nzuri ni kumpa busu.

Bahati mbaya ni kwamba wanandoa wengi wameshikwa na kunaswa na mtego wa u-busy hadi imefika wanasahau kuwabusu wapenzi wao.
Niambie wewe unayesoma sasa hivi hapa umembusu mke wako au mume wako lini?
Nahisi umesahau!
Plainly; mahusiano yanahitaji kazi, hasa kwa huyo special someone wako in your life kama ulifanya kazi kumpata kwa nini sasa ulegeze kamba, kaza uzi hakikisha uzi uleule uliotumia kumpata ndo huohuo unatumia kudumisha penzi na si kudumu tu bali linakuwa sustainable.

Kubusu hujenga intimacy kati ya mke au mume pia hufanya bonding iwe strong na kuhufanya wewe mwenyewe ujisikia vizuri na afya njema.

NINI FAIDA ZA KUBUSU KIAFYA?
Busu ni afya kwa meno yako, wataalamu wamefanya tafiti na kugundua kwamba busu kuzuia plague kujijenga kwenye meno na hii ina maana utapunguza safari kwa daktari wa meno.

Busu ni afya kwa moyo wako (heart) kwani wakati wa kubusiana mnazalisha adrenaline ambazo husababisha moyo kuongeza speed na damu kwenda sehemu zote za mwili.

Kila mwanaume au mwanamke ambaye humuaga mwenzake asubuhi kwa busu utafiti unaonesha anaongeza miak 5 zaidi kuishi duniani.
Kama huwa hubusu wakati unaagana na mwenzi wako asubuhi unajipiga panga miaka 5 kuishi.

Kubusu hukuongezea self esteem na kujisikia upo appreciated kwani busu ni tamu na raha.

Mabusu hupunguza kuzeeka kwani mnapobusiana huhusisha misuli zaidi ya 29 kwenye eneo la mashavu na shingo.

Kubusu huchoma calories kati ya 6 – 12 na mkiongeza na love making huweza kufikia 300 na utajisikia raha.

Kubusu huondoa stress, huweza kutoa ocytocin, homoni ambayo hufanya mtu kujisikia vizuri.

Hakikisha unapobusu ni zaidi ya sekunde 10 ili kupata matokeo.

Hivyo basi wewe na mpenzi wako go ahead, kwa afya na furaha sherehekea kila siku kwa kupigana mabusu.

Saturday, May 28, 2016

MAJUKUMU YA VIONGOZI.

1.MWENYEKITI/MAKAMU WAKE.

*Ndiye mhimili wa utendaji na msemaji mkuu wa GROUP.

*Kuongoza mijadala ktk mikutano na kupitisha na kuhidhinisha dondoo za mikutano.

* Kutoa uamuzi wa mwisho kadri ya busara yake pale mawazo yanapogongana.

*Kufuatilia itekelezaji wa maazimio ya mikutano.

*Kuwa kiungo kati ya Viongozi na membesr wengine.

*Kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbalu.


2.KATIBU/NAIBU WAKE.

*Kuwa mtendaji mkuu na kumshauri mwenyekiti katika masuala yote ya kiutendaji.

*Kuandaa dondoo za mikutano na kuitisha vikao.

*Kutunza kumbukumbu zote.

*Kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mikutano ikiwa ni pamoja na kuandaa taarifa mbalimbali na kuziwasilisha sehemu husika.

3.MSIMAMIZI WA NIDHAMU

Kusimamia na kuhakikisha kanuni na taratibu zinafuatwa.

*Kutoa adhabu stahiki kwa waliofanya makosa bila kuonea.


4.KAMATI YA MASHAURIANO.

*Jukumu kubwa ni kuhakikisha wanawashauri vema Viongozi kwa masuala mbalimbali yahusuyo Group.


5.MAADMIN..

*Kulifanya group kuwa acitve kwa kutoa mada au masomo mbalimbali.

*Kubuni mikakati mipya ya kuongeza uhai wa Group.

*Kutoa ushauri kwa Members wenye matatizo mbalimbali kwa kutumia busara.

*Kutoa Mada na kuielezea kwa ufasaha ili members waielewa.



NAOMBA TUWAPE USHIRIKIANO WA KUTOSHA ILI TULIWEKE GROUP LETU KWENYE LEVEL NYINGINE.

ASanteni sana na Mungu Awabariki.....Imeandaliwa na Dr.Mwillongo- ADMIN MKUU

TUZUNGUMZIE MAHUSIANO.

VIONGOZI WA GROUP:-

1.DR.NAYTHAM - MWENYEKITI.

2. SIMON. - M/MWENYEKITI.

3. PAUL - KATIBU.

4. OLYMPIA - N/KATIBU.

5. HOLINESS - MSIMAMIZI WA NIDHAMU.

KAMATI YA MASHAURIANO

1. FRANK JOHN

2. FEDILIA

3.EDMUND.

4. MAMA VICK.

5. SHANGWE.


*MAADMIN.

1.BEATRICE BAZIL.

2. MANLUCA.

3.FLORA MRAMBOA.

4. MERRY. (SUPERWOMAN)