Thursday, February 4, 2016

SWALI

Habari kaka Jeffy na wadau wote .
Tunashukuru sana kwa kutuelimisha katika suala zima la mahusiano.
Mimi nimezaliwa katika familia ambayo suala la sex halikuwa topic ambayo inaweza kuongelewa kwa namna yoyote ile.
Kutokana na hayo malezi (Christian) inakuwa ngumu sana kwangu kuwa wazi kumueleza mume wangu kwamba nahitaji tendo la ndoa hii ina maana hata kama ninahitaji huwa namsubiri yeye aanze hata hivyo katika kusoma Mada zako nimejifunza kwamba ni vizuri kwa mke wakati mwingine kulianzisha (naamini umeelewa nina maana gani).
Je, nifanyeje ili niweze kujisikia rahisi kumwambia au kumweleza!

No comments:

Post a Comment