Sunday, January 31, 2016

+ KATIBA YA JUMUIYA YA BIKIRA MARIA MAMA WA ROZARI TAKATIFU +

1.Ni wajibu wa kila mwanajumuiya kuhudhuria siku ya kusali jumuiya hii ni kwa waamini wote walio na umri kuanzia miaka 14.

2.Mwanajumuiya ambae hatahudhuria Jumuiya kwa kipindi cha wiki 4,bila kuwepo kwa taarifa yoyote Jumuiyani atahesabika kama amejiondoa kwenye Jumuiya.Hivyo Jumuiya haitahusika na chochote ikiwemo maombi yoyote ya huduma za kiroho kwa mwanajumuiya huyo.Mwanajumuiya huyu atapaswa kuomba tena kujiunga na jumuiya kwa kujaza fomu na kujieleza kwa viongozi ikiwa atahitaji kurudi tena.

3.Jumuiya itatoa kiasi cha shilingi 20,000 ikiwa ni mchango wao wa pole kwa mwanajumuiya atakaefiwa na wategemezi wake ambao ni Baba,Mama,Mume,Mke ama Mtoto.

4.Jumuiya itatoa kiasi cha shilingi 20,000 kwa mwanajumuiya atakaepata mtoto (kujifungua) ikiwa ni pongezi zao.

5.Jumuiya itatoa kiasi cha shilingi 20,000 kwa mwanajumuiya atakayeumwa zaidi ya wiki 2,ila ikiwa tu yupo hospitalini lakini pia kwa aliefanyiwa operation.

6.Jumuiya itatoa kiasi cha shilingi 50,000 kama mchango wao wa pongezi kwa mwanajumuiya atakayefunga ndoa.

N:B:- Michango hiyo itatoka kwa wale wanajumuiya ambao wanashiriki kutoa michango hiyo.

Saturday, January 30, 2016

VIONGOZI WA VYAMA.VYA KITUME.

UWAKA.

1.MWENYEKITI.

DEUS LYIUKI.

2.MAKAMU MWENYEKITI.

REMMY MUSHI.


3.KATIBU.

VICENT KATABI.

4.NAIBU KATIBU.

BAHATI MWINGIRA

5.MWEKA HAZINA.

ANICET BULETA.



WAWATA.

1.MWENYEKITI.

SIKUDHANI ABDUL.

2.MAKAMU MWENYEKITI.

NEEMA MBWANIRUA.

3.KATIBU.

VIVIANI MWINUKA.


4.NAIBU KATIBU.

OLIVER AUGUSTINO.

5.MWEKA HAZINA.

JOSEPHINA OSCAR.



VIJANA.

1.MWENYEKITI.

JASMIN MBWANIRUA.

2.MAKAMU MWENYEKITI.

COSMAS MWINGIRA.



KAMATI YA AFYA.

1.MWENYEKITI.

YASINTA TENDEGA.

2.MAKAMU MWENYEKITI.

IRENE MALLYA.

3.KATIBU.

ZUBEFA NYWAGE.

4.NAIBU KATIBU.

ALFREDA MKWANGO.

5.MWEKA HAZINA.

PAULINA SIMON.

TUMSIFU YESU KRISTO.!?

Leo Tarehe 30-01-2016,Jumuiya ilisali nyumbani kwa Anicet Buleta.

Agenda kuu ya leo ilikuwa ni Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya na Viongozi wa Vyama vya Kitume watakaoongoza kwa kipindi kingine cha Miaka 3.

Wasimamizi wa Uchaguzi ambao waliteuliwa na Parokia walikuwa ni:-

1.THEOBALD CHINANGUILE

2.DONALD MAKONDA

Waliochaguliwa walikuwa ni kama ifuatavyo:-

VIONGOZI WA JUMUIYA.

1 MWENYEKITI - SIMON JOHN.

2.MAKAMU MWENYEKITI - GLORIA MARTINI.

3.KATIBU - NEEMA GODWIN.

4.NAIBU KATIBU.
DANIEL MINJA.

5.MWEKA HAZINA.
CALISTUS NGULIMI.

Sunday, January 24, 2016

Jambo la msingikatika swali lako ni kwamba kawaida (mara ngapi sex iwe kwa siku, wiki au mwezi) ni suala la wewe na mume wako kuzungumza, kuelewana na kukubaliana au wewe mwenyewe binafsi kufika mahali ukafahamu kwamba mume wako na wewe kila mmoja ana hamu ya kimapenzi kiasi gani kwa siku au wiki au mwezi kwa maana kwamba kumfahamu mwenzako uhitaji wake na kila ndoa duniani ipo tofauti kwa maana kwamba wengine hufanya sex kila siku, wengine kwa wiki mara 1 au 2 au 3 na wengine kwa mwezi mara 1 au 20 na wengine hata wakifanya sex kwa mwaka mara 1 wanaona sawa tu.

Kujihusisha na sex mara kwa mara kwa wanandoa hutokana na afya, emotions, kubadilika kwa maisha, stress, depressions, migogoro, kufiwa na kazi na uchumi hata watoto nk na kiwango cha kuhitaji sex hakiwezi kuwa sawa au juu maisha yote kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya sex na akili.
Kama mume wako ni mkali inawezekana hormones zake za testosterones zimepanda sana zinahitaji release na njia muafaka kwake ni wewe kuwa available (kumpa sex).
Inawezekana huko kazini boss anamkalia sana mume wako kiasi kwamba akirudi nyumbani anahitaji mwanamke ambaye anaweza kumfariji na kumpa caring na attention kubwa kwake.
Ndoa ni kufanya kila kitu pamoja, kuelewana, kuzungumza na kuwasha moto wa kimapenzi ili kila mmoja aridhishwe kimapenzi na wewe ni mwanamke ambaye ni halisi kwa ajili yake.
Hivyo unahitaji kuwa mwangalifu kusoma namna upepo unavuma hapo nyumbani, ukiona ana dalili kwamba anakuhitaji kimapenzi unahitaji kuwa available bila kujali mnafanya sex mara ngapi kwa wiki, kwani suala la msingi si mara ngapi kwa siku au wiki bali unaridhika au kuridhishwa kiasi gani na mume au mke wako.
Wewe ni mwanamke na una advantage kubwa kwani ni rahisi sana kumsoma mume wako na pia hata kama alikuwa hataki sex na wewe unahitaji bado ni rahisi sana kuwasha umeme (kumfanya awe stimulated) na kuhakikisha Uume wake unashawishika kukubali ombi lako kwani kwa urembo wako na uzuri wako hakuna kisichowezekana.

Wednesday, January 13, 2016

KWANINI YAWE MAPENZI YA SIRI?

Bila shaka utakuwa unaelewa vizuri nikizungumzia mapenzi ya siri. Inawezekana umewahi kuwa katika aina hii ya uhusiano, umewahi kusikia au kushuhudia watu wawili wanaopendana, wakiendesha uhusiano wao kwa siri kubwa.

,kwa nini kuna baadhi ya watu hupenda kuishi kwenye uhusiano wa siri?
Najua wapo wengi ambao wapo kwenye uhusiano wa siri na wanazo sababu zinazowafanya waishi kwenye aina hiyo ya uhusiano, lakini je, kama unampenda, na yeye anakupenda kwa dhati, kuna haja gani ya kuishi kwenye uhusiano wa siri?

MAPENZI YA SIRI YANAVYOKUWA
Katika aina hii ya mapenzi, kila kitu wanachokifanya wahusika, kinakuwa kimetawaliwa na usiri wa hali ya juu. Uko naye, siku zinazidi kuyoyoma lakini humfahamu rafiki yake hata mmoja na yeye hamfahamu rafiki yako au ndugu yako hata mmoja.

Hata watu wenu wa karibu wanaowazunguka, hakuna hata mmoja anayejua kwamba nyie ni wapenzi. Mazungumzo yenu mnayafanya kwa siri sana, kukutana kwenu pia kunakuwa ni kwa kuibia sana, tena kwenye maeneo ya vificho.

Hata kama mnafanya kazi ofisi moja, hamuoneshi dalili yoyote ya kuwa wapenzi, hakuna ukaribu kati yenu na kila kitu kinatawaliwa na usiri. Muda pekee mnaokuwa huru, ni pale mnapokuwa peke yenu, yaani wewe na yeye tu.
Hata kama mnataka kutoana ‘out’, mpo radhi msafiri kwa umbali mrefu kwenda sehemu ambayo hakuna anayewafahamu.

DALILI MBAYA
Yawezekana umejikuta tu katika mkumbo wa mapenzi ya siri! Yaani mwenzi wako ndiye anayekulazimisha muishi aina hiyo ya maisha lakini ndani ya moyo wako unaona kama unaidhulumu nafsi yako.

Unatamani kila mtu ajue kwamba ninyi ni wapenzi lakini mwenzi wako anakukataza kufanya hivyo. Pengine hata anakupa vitisho kwamba utakapotoa siri ya uhusiano wenu, huo ndiyo utakuwa mwisho wa mapenzi yenu.

Shtuka! Chunguza kwa kina kwa nini mwenzi wako anataka muishi maisha ya mapenzi ya siri wakati kila siku anakwambia kwamba anakupenda na yupo tayari kufanya chochote kwa ajili yako. Mara nyingi, uhusiano wa siri huwa ni dalili mbaya kwa wahusika! Kwamba lipo jambo ambalo analificha na ndiyo maana anataka muwe wapenzi kwa siri.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazofanya mtu apende kuwa na uhusiano wa siri na mwenzi wake.

1. AMEOA/ AMEOLEWA
Sababu kubwa ya kwanza inayowafanya wengi wapende kuwa na uhusiano wa siri na wenzi wao ni kwa sababu wanakuwa wapo kwenye ndoa halali lakini kwa sababu ya tamaa zao, wanaamua kuchepuka. Katika kuchepuka huko, hawawaambii wenzi wapya ukweli kwamba tayari wanao wake au waume zao halali.

Wanawadanganya kwamba wapo singo ili wawatumie kimapenzi na watakapomaliza haja zao ndiyo wawaeleze ukweli na kuvunja mapenzi yao. Upo ushahidi wa wanawake wengi ambao walitongozwa, wakakubali kuanzisha uhusiano wa siri na wanaume na kukaa nao kwa kipindi kirefu lakini baadaye wakaja kugundua kumbe wao ni ‘spea tairi’.

Vilevile wapo wanaume ambao wameingizwa mkenge kwa kuingia kwenye uhusiano wa siri na wanawake, wakiwahudumia na kuwatimizia kila kitu lakini kumbe nyuma ya pazia ni wake za watu.

2. ANA MICHEPUKO MINGI
Sababu nyingine inayosababisha wengi wapende kuishi na wenzi wao kwa usiri, ni tabia ya umalaya au uhuni anayokuwa nayo mtu. Kwamba katika sehemu hiyohiyo moja, wewe unadhani uko peke yako lakini kumbe kuna wenzako kadhaa unapanga nao foleni. Kwa kuwa kila mmoja anatunza siri, inakuwa vigumu kujuana.

Wednesday, January 6, 2016

MAMBO MUHIMU YANAYOMPA HAMU MWANAMKE.

Kuna dalili za mwanamke anapotaka ngono.

Kwanza kabisa nikujulishe kuwa kitaalam mwanaume huwa anawaza ngono kila baada ya sekunde sita huku akiwaza mahala pa kufanyia tendo hilo wakati mwanamke huwaza ngono kila baada ya sekunde tisa na akikubali kuvua nguo ni lazima awe na sababu za msingi.

‘’Mimi sijisikii kufanya mapenzi’’ hii ni moja kati ya kauli ambazo wanaume huambiwa na ukisikia hivyo ujue si peke yako unayeambiwa hivyo na hii ni kauli inayolalamikiwa sana na wanaume wengi ambapo baadhi yao wamediriki hata kuchepuka wakidhani wenzi wao wamewachoka.

Wanawake wanapagawa na huhitaji kufanya mapenzi kuliko wanaume wengi wanavyodhani na ukijua mazingira hayo hautamwacha mwanamke wako,naye hatatamani mwingine kwasababu wanawake wanajieleza wazi kuwa katika mazingira nitakayoyataja hapa chini yakifuatwa wanajisikia raha mno…

1.      MFURAHISHE.
Hali yeyote ya furaha kupita kiasi inamfanya mwanamke kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufanya mapenzi bila kizuizi chochote.

2.     BAADA YA KUGOMBANA.

Kugombana ninakozungumzia hapa ni kule kwa pande mbili mnakwazana na baadaye kila upande ukatoa dukuduku zake hata kama kwa kufikishana kwa wakubwa kwa nia ya kupata muhafaka na baada ya hapo hakuna kitu kizuri cha kubadilisha upepo huo zaidi ya kukumbatiana, kubusiana kwa huba huku mkiziamsha hisia zenu.

Ukiona hata kama mwanamke wako analia au ameghafirika kwelikweli, mwache anyamaze au mnyamazishe huku ukimbembeleza hata kumfuta machozi kisha …….hapo tatizo linaisha na wakati huo wote kwa pamoja mtafurahia tendo hilo.

3.     KIPINDI CHA "HEAT PERIOD"...14 DAYS

Hiki ni kipindi cha joto kwa mwanamke, ni kipindi cha aina yake katika mahusiano ambapo mwanamke anakuwa na hisia nyingi wakati mayai yanapotungwa.

Hivyo zikiwa zimepita wiki tatu baada ya kumaliza Afya yake kisha damu kukauka’’ wakati huu ni muhafaka kufanya mapenzi na hata kama mwanaume ni mbishi kiasi gani au umechoka mwanamke atakuamsha na kukutega na mara nyingine atakueleza kuwa anataka.

4.     MAPENZI YA MBALI.

Mapenzi ya mbali yanaweza kuwafanya mkawa na maisha yasiyokuwa na migogoro ya mara kwa mara huku kila mmoja akiwa anamtamani mwenzake na kitu pekee kwa wakati huu wa utandawazi kinachoweza kuwaunganisha zaidi ni simu na internet.

Mkikutana siku hiyo kila mmoja anamtamani mwenzake na kama ni asubuhi mtaona siku haiendi haraka hasa kwa wale wenye familia na kama mtakuwa wawili katika chumba ama nyumba hiyo aaaaaaahhhhh hiyo niwape hongera kwasababu hamtakawia hata sebuleni.......

5.     WIVU

Ninachozungumzia hapa si ule wivu wa kijinga bali nazungumzia wivu wa mwanamke anayejitambua na kujiamini kuwa anamtii, kumnyenyekea na kumshauri kwa hekima mwanaume wake lakini anapata wivu anapoona mwanaume huyo yupo na mwanamke mwingine hata kama si katika mahusiano. Si unajua kila mtu ana moyo wa nyama? Hasa ukipenda.

Mwanamke anapoona mwanaume wake ananyemelewa na mwanamke mwingine na kumshawishi kimapenzi huona wivu sana na wanawake wanaojitambua badala ya kufoka huamua kuwaonyeshea wanaume wao kitandani kwa kuwapa mapenzi motomoto huku wakionyesha staili na kuonyesha kujiamini kuwa ni wazuri kila upande yaani sura, maumbile na hata kitandani kuliko wale wanaomnyemelea.

Hapa siruhusu wanaume kuwa vicheche ama kuambatana na wanawake wengine bila sababu eti tu unataka mwanamke wako akuonee wivu hapana hii ni mbinu ya kuotea maana kumrusha roho mtoto wa mwanaume mwenzako si vema.

6.  MWANAMKE KUJINYIMA.

Kadri mwanamke anavyozidi kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi ndivyo anazidi kupata ashki ‘’Nyege’’ na mwanaume unapompata mwanamke aliyekaa muda mrefu hakika utafaidi na yeye pia atakuweka kwenye historia maana atajisikia raha sana baada ya tendo hilo.

Na mwanamke wa namna hii haitoshi kuwa mmefanya tendo la ndoa siku moja huyu atahitaji walau siku mbili vinginevyo ukimwacha atachepuka ingawa ni wachache wanaoamua kufa kisabuni na kuamua kutumia maji ya moto kujikanda.

7. MAWAZO.

Mwanamke ambaye amekuwa na mawazo kwa muda mrefu akihitaji faraja na akakosa hatimaye Mungu na malaika wake wakamwangazia nuru na kujikuta mikononi mwa mwanaume anayeweza kumpa mapenzi yatakayomfariji hakika mwanamke hufurahia tendo hilo ambalo anahisi linakata kiu yake na kushusha pumzi.

8.     MBUNIFU.

Wanaume wengi wanawanyima uhuru wa mazingira wanawake zao huku wakihoji ‘’ameyapata wapi haya’’ nakushindwa kujua kuwa huo ni moja ya mtego wa kutaka mapenzi.

Mwanamke anaweza kukutaka mfanye mapenzi jikoni, bafuni, sebuleni kwenye kiti au popote pale na kama amekupagawisha vizuri katika penzi la jikoni kuna siku mnaweza kujikuta mkiacha chakula kikiungulia huku nyie mkiwa mnatoa jasho la Afya na hapo mwanamke atafurahi kwasababu mtego wake wa kuku haujanasa chui.

9. MUZIKI NA KINYWAJI.

Kucheza muziki na wengine wale ambao wanapata kidogo kinywaji ni moja ya mambo ambayo yanasisimua mwili na kuamsha hisia za mahaba kwa mwanamke.

Hapa kwa mwanaume unaweza kumchukua mwanamke wako na kwenda naye kwenye kumbi za muziki.

Wakati mnacheza jaribu kugusana ama kupapasana taratibu hapo mwanamke yeyote mradi akikubali kupapaswa, mambo yanakuwa si mambo.

Sunday, January 3, 2016

SIMU ZA MKONONI...

Mwanaume au hata mwanamke ukiona simu yake ina password au anaichunga sana hata akiwa nyumbani, ujue hapo hakuna usalama.Mtu aliyeitengeneza kusudio lake kubwa lilikuwa kurahisisha mawasiliano si kingine. Lakini wanadamu wenye mioyo dhaifu tumeitumia kama kichaka cha kuficha maovu yetu.
Sasa hivi ndani ya nyumba simu imekuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani, asiye muaminifu uilinda simu yake kama ikulu.
Sasa hivi ndani ya nyumba zetu inaonyesha jinsi gani zimepoteza uaminifu kila mmoja analinda simu yake kuliko hata wivu kwa mwenzake.
Imekuwa kila mmoja anamwinda mwenzake alale ili aipekue simu, kwa vile ni mzoefu hata ukibahatika kuipata utakuta uchafu wake amefuta ili kupoteza ushahidi.
Ukiona hivyo mnakuwa mnaishi kwa mazoea lakini fahamu hakuna upendo ndani ya nyumba yenu na kuvunja ile ahadi ya kuishi kwa upendo na uaminifu katika ndoa.
Unaweka password unamuonyesha nini mwenzako? kama mwanaume unamuonyesha kabisa mkeo kwamba una wengine zaidi yake hapo unamfundisha nini mkeo, akilipa kisasi umlaumu nani?
Nimekuwa nikisema kila siku kuhusu uaminifu ili tuangalie unachokifanya ni sahihi na ndiyo mapenzi?
Nilielezea mapenzi ni kupendana kuheshimiana kuoneana huruma kujaliana na uvumilivu.
Nilielezea mapenzi ni kupendana, kuheshimiana, kuoneana huruma, kujaliana na kuvumiliana. Ukiwa na mapenzi lazima utakuwa na vitu hivi kwa mwenzako, pia utakuwa muwazi kwake na mkweli ili kufanya muweze kuishi bila mmoja kuwa na mashaka na mwenzake.
Wapendanao siku zote hulinda heshima yao kwa kila mmoja kuilinda ya mwenzake, pia kuwa wawazi ili chochote kitakachokwenda kinyume, kiulizwe na kupatiwa majibu sahihi bila kujiumauma. Pia huwa hawana mipaka kuanzia katika miili yao na vitu vyote kwa vile huamini wao ni kitu kimoja, hivyo hawafichani kitu.
Watu kama hawa simu si chanzo cha matatizo, bali ni chombo cha mawasiliano, hakuna mtu wa kuificha simu yake wala kuweka password na kila mmoja ana uhuru wa kuishika au kuopokea ya mwenzake.
Nina imani somo langu limesomeka vizuri, sasa tunarudi kwenye mada ya leo kwa kuuliza swali, sifa nilizozieleza kuhusu mapenzi, je, wewe unazo au mwenzako anazo? Je, simu katika nyumba yenu inatumikaje? Ni chanzo cha migogoro au ni chombo cha mawasiliano ambacho kinaachwa popote bila masharti yoyote?
Tutumie simu kama chombo cha mawasiliano, hata kama si muaminifu katika uhusiano, si lazima mwenzako ajue jinsi gani unavyomdharau kupitia simu.
Simu isiwe chanzo cha migogoro na kuvunja nyumba zetu ambazo sasa hivi zimeingia mdudu ambaye ameonyesha jinsi gani tusivyo waaminifu, kitu ambacho kimeongeza ukosefu wa amani katika ndoa zetu.
Tuwe wawazi na wakweli kwa wenzetu, tuone aibu kuonyesha kwa vitendo sisi si waaminifu. Kama ulijua wazuri kuliko mwenzako wapo wengi, ulikaa naye kwa sababu gani?