Sunday, January 24, 2016

Jambo la msingikatika swali lako ni kwamba kawaida (mara ngapi sex iwe kwa siku, wiki au mwezi) ni suala la wewe na mume wako kuzungumza, kuelewana na kukubaliana au wewe mwenyewe binafsi kufika mahali ukafahamu kwamba mume wako na wewe kila mmoja ana hamu ya kimapenzi kiasi gani kwa siku au wiki au mwezi kwa maana kwamba kumfahamu mwenzako uhitaji wake na kila ndoa duniani ipo tofauti kwa maana kwamba wengine hufanya sex kila siku, wengine kwa wiki mara 1 au 2 au 3 na wengine kwa mwezi mara 1 au 20 na wengine hata wakifanya sex kwa mwaka mara 1 wanaona sawa tu.

Kujihusisha na sex mara kwa mara kwa wanandoa hutokana na afya, emotions, kubadilika kwa maisha, stress, depressions, migogoro, kufiwa na kazi na uchumi hata watoto nk na kiwango cha kuhitaji sex hakiwezi kuwa sawa au juu maisha yote kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya sex na akili.
Kama mume wako ni mkali inawezekana hormones zake za testosterones zimepanda sana zinahitaji release na njia muafaka kwake ni wewe kuwa available (kumpa sex).
Inawezekana huko kazini boss anamkalia sana mume wako kiasi kwamba akirudi nyumbani anahitaji mwanamke ambaye anaweza kumfariji na kumpa caring na attention kubwa kwake.
Ndoa ni kufanya kila kitu pamoja, kuelewana, kuzungumza na kuwasha moto wa kimapenzi ili kila mmoja aridhishwe kimapenzi na wewe ni mwanamke ambaye ni halisi kwa ajili yake.
Hivyo unahitaji kuwa mwangalifu kusoma namna upepo unavuma hapo nyumbani, ukiona ana dalili kwamba anakuhitaji kimapenzi unahitaji kuwa available bila kujali mnafanya sex mara ngapi kwa wiki, kwani suala la msingi si mara ngapi kwa siku au wiki bali unaridhika au kuridhishwa kiasi gani na mume au mke wako.
Wewe ni mwanamke na una advantage kubwa kwani ni rahisi sana kumsoma mume wako na pia hata kama alikuwa hataki sex na wewe unahitaji bado ni rahisi sana kuwasha umeme (kumfanya awe stimulated) na kuhakikisha Uume wake unashawishika kukubali ombi lako kwani kwa urembo wako na uzuri wako hakuna kisichowezekana.

No comments:

Post a Comment